Ni nani ameiloga bara la Africa?
Habari kutoka nchini Tanzania zinazo aminika,kufuati uchunguzi wa huu wa 2020,inasemekana kwamba bwana Dr.Pombe Magufuri John,atashinda uchaguzi wa mwaka huu,kwasababu amejaribu kupiga vita upinzani wake bila kujali shelia inayo ruhusu upinzani kupata uhuru wa kupiga siasa ndani nchini Tanzania.
Bwana Magufuri baaada ya kuchaguliwa kama Rais wa jamhuri ya Tanzania,alijaribu kuweka kufuri pande zote za kisiasa,ambapo anafunga wana Habari,bira kusahahu wanasiasa ameiga mwendo wa Yoweri Kaguta Museveni na Paul Kagame wanao ongoza nchi zao wakitumia mkono wa chuma.
Wachanganuzi wa kisiasa wanasema kwamba uchanguzi wa rais nchini Tanzania utakao fanyika tarehe 20 octoba,niwazi kwamba Magufuri atashinda kwasababu amelemea upinzani sana kiasa kwamba uhuru nchi ya Tanzania ilikuwa imezoa,kwa sasa ni ndoto katika nchi ya Tanzania.
Kwa miaka kadhaa iliopita wa Tanzania ni watu ambao walikuwa wamezoea uhuru na haki,kadiri miaka inaenda ikiyoyoma,ni dhahili kwamba uhuru walio kuwa nao unapotea kwasababu ya utawala wa kimabavu wa chama cha mapinduzi CCM.
Licha ya kwamba uchumi wa Tanzania umeongezeka kwa kiasi kikubwa,lakini upande wa kisiasa imerudi nyuma sana.Dunia yote imeshuhudia utawala wa Magufuri,ambapo hata virus ya Covid 19,amejaribu kuficha takwimu ya walio ambukizwa virus hivyo.Hata inasemekana kwamba kuvaa mask ni makosa makubwa atakae patikana akiwa ameivaa mask (kalinda mdomo) atachukuliwa hatua za kishelia.
Kwa sasa wa Tanzania wanaendelea kufa kwasababu ya virus vya corona virus.Magufuri alipo ona kuwa uchaguzi unakaribia,na pia ugonjwa wa virusi vya covid 19 vimeidhofisha dunia nzima,aliogopa kuwa anaweza kushindwa uchaguzi,na akose njia ya kuiba matokeo ya uchaguzi katika harakati hizo aende nyumbani akiwa ameongoza mhula mmoja.
Baada ya bwana Magufuri kuingia uongozini,amaua uhuru Tanzania na demokarasiya ya kitanzania,hata kama alichaguliwa na wananchi,lakini utawala wake umekuwa wa kimabavu(dictatorship)ni kama hakuchaguliwa na wananchi.Inabainika kwamba atakapo shinda uchuguzi huu utakao fanyika octoba 20,2020,baada ya miaka (5) mingine demokalasiya nchini Tanzania ataacha ameizika kaburini!??
Nikiandika nakara hii,imenikumbusha Habari nilizo zisoma katika gazeti la bbc,Habari zilikuwa zinaeleza namna rais Museveni wa Uganda akatakavyo shinda uchaguzi mwaka ujao wa 2021 mwezi wa pili.Nilishangazwa sana mwandishi alipomalizia Habari yake akisema kwamba hata bwana Museveni akatakapo maliza miaka (40) kwa uongozi wake,inawezekana atajiongeza miaka mingine (5) mpaka atakapo kufia uongozini.
Ni kama kunamashindano kati ya Yoweri Kaguta Muveni na bwana Paul Kagame wa Rwanda,ambapo na yeye alipewa zawadi ya kuongoza mika Zaidi ya (40); wawili hao wanatarajia kuachia utawala Watoto wao,General Keinerugaba amabye kwa sasa ni jemedali mkuu wa majeshi nchini Uganda,baba yake anataka kumuachia utwara ni kama Uganda imegeuka kuwa shamba la familiya.
Vivyo hivyo rais wa Rwanda Paul Kagame,na yeye anataka kuachia utawala kijana wake LT.IVAN CYOMORO,ambaye kwa sasa ndiye anaye linda usarama wa baba yake.Ikumbukwe kwamba hawa wawili wamechukuwa uongozi kwa njia ya kimabavu hat ana baada ya vita,wamekataa ku kubali demokarasiya nchini mwao,wanao jaribu kusimama uchaguzi wanafungwa na kuwekewa madhambi yasiyo na uhusiano na mshutumiwa.Ni dhahili kwamba mikakati ya East Afrika Community EAC haitaweza kuafikiana na siasa za kimabavu katika ukanda huu wetu wa Afrika mashariki.
Habari za kuaminika za hivi karibuni,zinasema kwamba shirika la kimataifa WHO,baada ya kunyimwa msaada wa kifedha na nchi ya Mericani,Kagame aliweza kuchukuwa furusa hiyo,akapatia WHO kitu kidogo,ili watangaze kwamba Paul Kagame ameweza kudhatiti ugonjwa wa virus cya Covid 19,kwa mjibu wa kutengeneza jina ili awezeshwe kujipatia misaada ya kimataifa.
Ikumbukwe kwamba bwana paul kagame alikuwa mkuu wa ujasusi nchini Uganda akiongazwa na Yoweri Kaguta Museveni,baada ya vita vyilivyo chukuwa miaka (5) baada ya kumuondoa IDDY Amin DADA Miltoni Obote aliongoza nchi hiyo,ambapo Museveni hakukubali kuwa alishindwa uchaguzi.Ndiposa alirudi kichakani akamuondoa Obote,na akawa rais wa Uganda.Baada ya miaka (5) pia,walivamia nchi ya Rwanda iliyokuwa ikiongozwa na rais Habyarimana Juvenal,wakamung’o madarakani Kagame akachukuwa nyidhifa zilizomwezesha kuwa rais baada ya kumua kiongozi wake General Gisa Fred Rwigema,na viongozi wengine wengi takribani (41) walio kuwa juu yake waliokuwa wanamzidi uzoefu wa kupigana.Lakini Habari zinasema kwamba yote hayo yarifanywa na Yoweri Kaguta Museveni aliye kuwa anatarajia atatumia kagame kuongoza nchi ya Rwanda ndani ya Paul Kagame.