HomePoliticsLouise Mushikiwabo anaye gombea muhura wake wa pili, ni kama atashindwa uchaguzi...

Louise Mushikiwabo anaye gombea muhura wake wa pili, ni kama atashindwa uchaguzi huu utafanyika baada ya siku mbili tu!

Serikali ya Rwanda imekataa ombi la Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, la kuitaka nchi hiyo kumuondoa mgombea wake, Louise Mushikiwabo, katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nchi zinazozungumza Kifaransa, OIF. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, amesema ombi hilo limekataliwa. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 16, huku kukiwa na mvutano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Louise Mushikiwabo, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Paul Kagame, anawania muhula wa pili dhidi ya wagombea wengine watatu, akiwemo Juliana Lumumba wa DRC. Wagombea wengine ni Coumba Ba wa Mauritania na Dacian CioloÈ™ wa Romania.

Kongo imetishia kujiondoa katika OIF iwapo Mushikiwabo atachaguliwa tena, ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23. 

Rais Macron yupo Phnom Penh, Cambodia, kwa ajili ya mkutano wa kilele wa OIF.

egretnewseditor@gmail.com 

 

RELATED ARTICLES
- Advertisment -
Google search engine

Most Popular

Recent Comments