Brussels: Umoja wa Ulaya leo umejadili njia zaidi za kuongeza kurejeshwa makwao wahamiaji wakati ambapo kundi moja la mataifa linaendelea na mpango wenye kuleta mgawanyiko wa kuwarejesha katika nchi nje ya Ulaya, wanaotafuta hifadhi ambao maombi yao yalikataliwa. Â
Mawaziri wa mambo ya ndani wa mataifa 27 ya Umoja wa UIaya wanakutana huko Luxembourg leo huku gumzo la kuwapinga wahamiaji likiwa limeshamiri Ulaya, kama ilivyothibitishwa na ushindi wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani mwezi uliopita.
Mawaziri hao wanatarajiwa kupitisha sheria mpya kali za Umoja wa Ulaya zinazozipa mamlaka nguvu pana zaidi za kuwazuia wahamiaji na kubuni maeneo ya kuwarejesha, kitu ambacho kundi moja la nchi hizo za Ulaya kinataka kulifanya.Â
Denmark, Ugiriki, Ujerumani, Austria na Uholanzi wamekuwa wakitafakari kubuni vituo kama hivyo, huku Rwanda ikisemekana kuwa juu ya orodha ya nchi zinazotaka kuwa na vituo hivyo.
 egretnewseditor@gmail.comÂ



