Home Justice Kanisa Katoliki walipa miliyoni 800,000 za kimalikani kwasababu ya unyanyasaji wa kingono

Kanisa Katoliki walipa miliyoni 800,000 za kimalikani kwasababu ya unyanyasaji wa kingono

0

Takribani manusura 1,300 wa unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanywa na viongozi wa Kanisa Katoliki wamekubali makubaliano ya fidia ya dola milioni 800 za Marekani na Jimbo Kuu Katoliki la New York (Archdiocese of New York).

Wanasheria wanaowawakilisha waathirika hao walisema makubaliano hayo ni miongoni mwa malipo makubwa zaidi kuwahi kufikiwa nchini Marekani katika msururu wa kesi za unyanyasaji wa kingono unaohusisha viongozi wa dini. 

Kundi la Jeff Anderson & Associates lilieleza hatua hiyo kuwa ni maendeleo muhimu katika harakati za kutafuta haki kwa manusura.

Mbali na fidia hiyo, Jimbo Kuu la New York limekubali kutoa nyaraka zinazohusiana na wahusika wa makosa ya kingono ndani ya Kanisa. Makubaliano hayo pia yanawaruhusu manusura kuendelea kudai fidia zaidi kutoka kwa kampuni za bima zinazohusika huku yakiepusha jimbo hilo kufilisika. Kanisa Katoliki nchini Marekani tayari limelipa mabilioni ya dola katika miaka ya karibuni kufuatia sheria mpya katika majimbo mbalimbali zilizowawezesha waathirika kufungua kesi za madai hata kwa makosa yaliyotokea miongo mingi iliyopita.

 egretnewseditor@gmail.com 

Translate »
Exit mobile version
Skip to toolbar