Home Top News Tahaluki yazidi kutanda katika mashariki ya kati

Tahaluki yazidi kutanda katika mashariki ya kati

0

Marekani inajiandaa kutuma wanajeshi na ndege zaidi nchini Israel katika wiki zijazo, ikiwa ni maandalizi ya uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo katika Mashariki ya Kati, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti.

Tovuti ya habari ya Walla, ikinukuu vyanzo vya usalama ambavyo haikuvitaja, imesema kuwa takribani wanajeshi 3,000 wa Marekani kwa sasa wako nchini Israel.

Majukumu yao ni pamoja na kuendesha mifumo ya ulinzi wa anga. Idadi hiyo pia inajumuisha marubani, wahudumu wa ndege, wataalamu wa usafirishaji na wanajeshi wanaohudumu katika makao makuu ya kijeshi.

egretnewseditor@gmail.com 

Translate »
Exit mobile version
Skip to toolbar